- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- orders@storymojaafrica.co.ke
Uamuzi Tata ni hadithi inayowahusu vijana wawili (Sula na Ja) wanaotoka katika matabaka tofauti. Sula ni binti mwoga anayetoka katika familia maskini inayoishi mtaa duni wa Bellington. Anazama katika vitabu anakosomea St Matthews, shule ya mabwanyenye ili kuficha taarifa ya familia yake. Anapojipata katika kikundi kimoja cha Kemia na mvulana maarufu shuleni, maisha yake yanachukua mkondo mpya.
Ja ni kimbelembele na mwana wa kipekee wa mama tajiri na baba anayeishi mbali nao. Maisha yake yanabadilika anapomtembelea baba yake ambaye ni mgonjwa mahututi. Aidha, anapata ana familia nyingine. Ufunuzi huu unabadilisha mtazamo wake wa maisha kwa jumla.
Sula na Ja wanapong'ang'ana kuelewa maisha yao ya ujana na ya familia zao, siku ya burudani ya kuadhimisha mwisho wa muhula imekaribia. Ja ataandamana na Sula kwenye burudani? Sula atakubali kuandamana na Ja? Soma hadithi kujua yatakayojiri.