- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- orders@storymojaafrica.co.ke
Soila anaijiunga na shule mpya akitazamia kwamba atapata fursa ya kupiga urafiki na kuingiliana vyema na wanafunzi wa shule hii. Haya yanajiri baada ya Soila kupata madhila makuu katika shule yake ya awali. Mandhari matulivu ya shule hii na mapokezi mema anayopewa na mwalimu mkuu pamoja na ‘dadaye wa shuleni’ yanamtia moyo na kumhakikishia kwamba amefika mahali pafaapo, yaani mambo hayatamwia tena mabaya jinsi yalivyokuwa katika shule ya awali. Matumaini yake yanaanza kudidimia pindi anapogundua kwamba wanafunzi wa shule hii wamejigawa katika matapo mbalimbali na ili mtu ajiunge na tapo lolote, lazima adhihirishe kwamba ana sifa zinazolandana na za wenyeji wa tapo hilo. Je, Soila atafanikiwa kujiunga na tapo lolote? Ana sifa za kumwezesha kuijunga na tapo gani?