- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- orders@storymojaafrica.co.ke
Mzi anatamani kitu kimoja: kulipiza kisasi. Anamchukia mpenzi wake wa zamani Ntombi. Tena anamchukia Olwethu kwa kumpokonya Ntombi. Mzi anaamini wawili hao walimshtaki kwa polisi kwa kushirikiana na genge la Zeki kuwaibia wakazi. Walinda usalama wamemwachilia Mzi kwa sharti moja; ajitenge na uhalifu, la sivyo arushwe gerezani. Awali, kabla ya polisi kumwonya, wanafunzi wa shule yake ya Harmony High walimwogopa na hata 'kumwabudu.' Hali sasa ni tofauti kwani wanafunzi wanamkejeli. Mzi anahisi upweke wa kupindukia kwa sababu amewekewa masharti makali na maafisa wa usalama. Marafiki zake, Vuyo na Prisilla wanamhimiza kurejelea uhalifu ili wanafunzi wamwogope. Mzi atafanikiwa kumkomoa Olwethu wakati huo kukwepa jela?